Marioo – Unanionea Lyrics

Marioo Unanionea Lyrics

Marioo – Unanionea

Marioo Unanionea Lyrics

Hivi kweli yupo
Mwenye roho mbaya kukushinda
Maana mi sijaona duniani

Hivi kweli yupo
Aso na haya kukushinda
Maana mie sijaona sijaona

We mtu gani uko radhi
Mwenzako niteketee
Wakati unajua dawa yake
Ni kumponya, nihurumie

Ama mtu gani aliefika
Akaongeza makeke
Na wakati anajua
Mi kwako ndo napona, we nihurumie

Mi najua mapenzi
Sio kwichi kwichi tu
Yanayonogaga mazoea
Nimekuzoea mmmh

Unanionea, mwenzako siwezi matukio mazito
Unanionea, unanipiga mie
Unanionea, unafanya nione mapenzi mabaya
Unanionea, lalalaa mmmmh

Na kama kuachana nakubali
Sawa fanya yako
Ila sio lazima unionyeshe uniumize

Au kisa unajua
Unaniacha bado nakuhitaji
Ndo unaona bora unikomeshe
Unilize eeeh

Ah poa poa, nishajua vya utamu
Vinakuwaga vya uchungu
Ili doa doa milima haikutani

Japo najua mapenzi
Sio kwichi kwichi tu
Yanayonogaga mazoea
Nimekuzoea mmmh

Unanionea, mwenzako siwezi matukio mazito
Unanionea, unanipiga mie
Unanionea, unafanya nione mapenzi mabaya
Unanionea, lalalaa

Unanionea, unanionea bure
Hata Bonga anajua unanionea
Chino anajua, unanionea
(It’s Lykos records)